CHADEMA WAWASHAMBULIA CUF KWA MAWE ARUSHA

CUF arusha

Bwana.Athuman aliepigwa jiwe

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

27/09/2012

WANACHAMA WA CUF KUPONDWA MAWE NA WAFUASIA WA CHADEMA ARUSHA.ONYO KWA CHADEMA

CUF Chama cha wanachi kinalaani kitendo cha wafuasi wa CUF  kupondwa mawe na wafuasi wa CHADEMA walipokuwa wakiendelea  na shughuli kutangaza mikutano inayoendelea Arusha .

Chama cha wananchi CUF kinasikitishwa na kulaani kitendo cha viongozi wa chadema mkoani Arusha kuwashawishi wafuasi wao kuwaponda mawe wanachama wa CUF wanaoendelea na mikutano ya kisiasa inayofanywa na CUF tangu mwanzo mwa wiki hii.Hii imedhihirishwa na maeno aliyoyatoa Godbless Lema juzi alipokuwa waapowahutubia wafuasi wa Chadema  kwenye viwanja vya Stendi ya Nduruma alisema kwamba CUF wametuvamia na kuwasihi wafuasi hao slogan ya “kamata mwizi men” sasa ianze kwa maana ya kuwafanyia vurugu CUF.Na ushahidi tuanao.

Hata hivyo wameshawishi vijana kugawana kiwanja cha Levorosi stendi ya Nduruma kwa kisingizio kwamba wanataka kuweka meza za biashara.Kiwanja hicho nchicho ambacho CUF tunantegemea kufanya mkutano wa hadhara siku ya Jumapili.

Leo asubuhi wanachama wa CUF wamepondwa mawe walipokuwa mtaa wa  Kilombero kata ya Levorosi wakiendelea na matangazo ya mkutano wa hadhara wakiwa kwenye gari la matangazo.Kutokana na vurugu hizo, gari la matangazo la CUF limepondwa mawe na  mwanachama mmoja aitwaye Athuman Abdurahman alipigwa jiwe jichoni na taarifa tumezifikisha polisi.

CUF kinaona Chadema kama chama kisichoweza siasa za ustahimilivu,hawajiamini na bado ni wachanga kisiasa.Hii inadhirishwa na kutoelewa maana ya demokrasia na uhuru wa Mtanzania kuamua kujiunga na chama chochote atakacho.Bado hawajakomaa kisiasa kama jinsi CUF ilivyokaomaa kisiasa,hatukudhuru chama chochote wanapofanya siasa maeneo mbalimmbali hapa nchini.

CUF inatoa onyo kali kwa viongozi wa Chadema kwamba hali hii ikiendelea wajue hawataweza kufanya shughuli zao sehemu yoyote Tanzania kwani uwezo wa kuwafanya tutakavyo tunao na kwasababu wameanza tuanaweza kumaliza.Ile NGANGARI kwa polisi tunaweza kuwahasishia wao wakose pa kukaa, ila hatupendi tufikie huko na kama wanabusara na ni wanasiasa kweli wenye nia ya kutumia hoja badala ya vurugu  kumkomboa mtanzania watafakari hilo.

CUF inaendelea kusisitiza,tutaendelea na shughuli za kisiasa mkoani Arusha hakuna wa kutuzuia na tutaendelea Oparesheni MCHAKAMCHAKA na mikutano itaendelea kufanyika na kama wao ni wababe kweli na wanatumia hoja ya vurugu waendelee na mipango yao ya hujuma na tutawafundisha siasa kwani bado hawajakomaa.

Imetolewa na

Naibu Mkurugenzi wa Habari ,Uenezi na Haki za Binadamu CUF.

Mh.Abdul Kambaya

Simu:0719566567

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s