CUF WATAKA AUREUS WATAIFISHWE KWA KUPORA MADINI NA KUKWEPA KODI

Jana naibu waziri  wa nishati na madini Bw.Masele  ameripoti kampuni  ya uchimbaji madini  ya  Aureus Ltd. ya Geita Mwanza  kutuibia watanzania dhahabu zetu zenye thamani ya takribani billion 12.7.Kampuni hiyo inayomilikiwa na Bw. Marc Rene Roelandts wa Barcelona, Hispania pia amedaiwa kutolipa kodi ya ya Mapato (PAYE),kutolipa VAT na kutorosha dhahabu takribani zaidi ya kilo 63.27.

CUF Chama cha Wananchi  kinaona kwamba huyu si mwekezaji bali mnyonyaji  tena aliyevunja mkataba wa nchi.Hali ambayo inatosha kwa serikali kuvunja mkataba,kutaifisha mali za kampuni hiyo na washirika wake wote wakiwemo watendaji wakuu ambao wengi wao ni wageni kutoka nje,kisha kuwafungulia mashtaka  na kuwafunga.

Tabia ya kuwapeleka mahakamani na kuendesha kesi kwa muda mrefu kisha kuwaachia imekuwa desturi ya Serikali yetu.Hii imefanya makampuni mengi ya madini  hasa ya nje yaendelea kuchota fedha na madini yetu bila wasiwasi kwani serikali ya CCM imeamua  kuwaachia wale huku wakishilikiana nao ilihali makabwela wa tanzania wakitaabika na umasikini.

CUF chama cha Wananchi kinashangazwa na serikali ya CCM kutochukua hatua nzito za kuwadhibiti wezi na waporaji hawa wa Aureus Ltd.

CUF chama cha Wananchi kinaitaka serikali mara moja mbali ya kuwafikisha mahakamani , kutaifisha mali za kampuni hiyo pamoja na fedha zote kwenye akaunti za nje na ndani ya nchi na wamiliki,pamoja na watendaji wa kampuni hiyo.Kwa vile wizi huu umezoeleka, kampuni zote za madini zifanyiwe ukaguzi wa kushtukiza kubaini wizi unaondelea kwenye migodi pamoja na kufanyia kazi taarifa zinazotolewa na Wananchi kuhusu wizi kwenye migodi.

CUF chama cha Wananchi kitatangaza hatua kali zaidi kwa serikali na migodi endapo mapendekezo haya hayatafanyiwa kazi.

Imetolewa na Abdul Kambaya(Naibu mkurugenzi Habari,Uenezi na Haki za Binadamu CUF)

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s