Kikao cha uongozi Baraza kuu CUF chaanza leo,Serikali yabanwa kuharibu nchi.

Bara za kuu la CUF -chama cha wananchi  linyewajumbe zaidi ya 60 kutoka kona mbalimbali za Tanzania bara na visiwani limeanza kikao chake leo ambapo litajadili mambo/ajenda mbalimbali zinazozohusu mustakabali wa Taifa kwa sasa na mipango mbalimbali ya chama nchi nzima.

Wakati wa ufunguzi wa mkutano huo mbele ya waandishi wa habari,makao makuu ya CUF Buguruni,Dar es Salaam mwenyekiti wa CUF taifa,

Naibu katibu mkuu bara Mh.Julis Mtatiro,Mwenyekiti Taifa Mh.Prof.Ibrahim Lipumba,Makamu mwenyekiti Mzee Issa Machano na Naibu katibu mkuu ZanzibarMh. Ismail Jusa Ladhu

Viongozi wa CUFkatika ufunguzi wa kikao cha Baraza Kuu kuanzia Kushoto Naibu katibu mkuu bara Mh.Julis Mtatiro,Mwenyekiti Taifa Mh.Prof.Ibrahim Lipumba,Makamu mwenyekiti Mzee Issa Machano na Naibu katibu mkuu ZanzibarMh. Ismail Jusa Ladhu

LIPUMBA MTATIRO
Mwenyekiti wa CUF Prof.Lipumba(kulia) akizungumza na vyombo vya habari

CUF
Naibu akatibu mkuu wa CUF bara(aliyesimama)akiwakaribisha wajumbe wa kikao na waandishi wa habari.

Profesa Ibrahim Lipumba amezungumzia mambo mbalimbali yanayohusu nchi kama ifutavyo;-

Mfumuko wa bei Mwenyekiti wa CUF prof.Lipumba amesema mwaka jana mfumuko wa bei ulikuwa zaidi ya 8% amabapo serikali ilidai unatokana na bei ya mafuta ya Petrol kupanda bei lakini  leo mfumuko wa bei  umepanda juu zaidi ya asilimia 18% na mfumuko wa bei za vyakula umepanda zaidi ya 24% hii yote ni kwa sababu ya matumizi makubwa ya kawaida ya serikali yanafanya bajeti kushindwa  kushughulikia mfumuko wa  bei kwani bajeti yake ni kiduchu mno.

Kilimo: Prof.lipumba alitanabaisha kwamba katika kila shilingi 100(mia) ya matumizi ya kawaida  ya serikali ya CCM  ni shilingi 3(tatu) tu ndiyo inatumika kuendeleza kilimo hapa nchini ndiyo maana kilimo kinazidi kushuka.

Mgomo wa Madaktari,Prof,lipumba amesema kwamba kwa mujibu wa sheria ya Tanzania wafanyakazi ambao hawapaswi kugoma ni pamoja na marubani,zimamoto,madaktari na wengineo kwa ajili ya usalama wa raia.Lakini madaktari wamegoma kwa sababu sera ya afya 2007 haikuwa na mpango kazi wa kuitekeleza na matokeo yake sekta ya afya imeyumba sana na madaktari hawaudumiwi ipasvyo.Lakini suala la kumtesa na kumdhuru Dk.Ulimboka ni fedheha kubwa kwa serikali kwani lazima itakuwa inajua anayehusika na Dk.Ulimboka hakustahili kufanyiwa hivyo.

Mchakato wa katiba mpya,Sio CCM wote wanaoikubali mchakato wa katiba mpya.Kuna kasoro kubwa kuhusu muda wa mchakato huu,Mchakato wa wa kuunda tume na sheria ya mchakato wa katiba mpya imechukua miezi 16 lakini tume imepewa miezi 18 kukusanya maoni ya katiba na kukamilisha mchakato mzima hii si sawa ni muda kidogo ambao kuna uwezekano wa katiba mpya kuongezwa muda na kukamilika zaidi ya mwaka 2015 vinginevyo itakuja katiba ya mfukoni ambayo imekwisha andaliwa na CCM.

Tume huru ya Uchaguzi.Kwa vile kunauwezekano mkubwa wa katiba mpya kuchelewa na kuwa baada ya 2015 kunahaja ya kuanzisha mchakato wa kuunda tume huru ya uchaguzi amabayo hata ikifika 2015 mchakato wa katiba mpya haujakamilika tunatakiwa tuingie kwenye uchaguzi tukiw na tumehuru ya uchaguzi isiyochakachua.

Sensa,Sensa  inaingia dosari kwa sababu serikali haijawa makini na mambo ya udini hivyo inapaswa kuwa makini hasa kuhusu takwimu zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya serikali za kuchanganya dini mbalimbali,serikali inapaswa kulikemea hili hadharani ili Wananchi wawe na imani na zoezi la sensa.

Prof.lipumba amesema kwamba matatizo yote hayo yanatokana na nchi kukumbwa na OMBWE LA UONGOZI unaosababishwa na seriakli ya CCM iliyochoka.Hivyo kwa muda wote huu wa siku mbili tutakuwa tukijadili namna ya kuikwamua nchi yetu kutoka hapa ilipokwama ili isonge mbele na namna ya kuimarisha na kuboresha mikakati ya dira ya CUF  kuelekea 2015.

 

 

 

 

 

 

Advertisements

3 thoughts on “Kikao cha uongozi Baraza kuu CUF chaanza leo,Serikali yabanwa kuharibu nchi.

  1. Watanzania tunatakiwa kumpa ridha prof lipumba ili awezekutmia uwezo wake wa kielimu,kiuchumi,ufahamu na huruma aliokuwanao kwa taifa lake kwa ujumla.kwani sasa tumeona huruma ya prof na uwezo wk.

  2. tunakitakia kikao cha baraza kuu mafanikio. Ili kimalizike kwa kuiletea nchi njia mbadala za kukomboa uchumi wa ktz

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s