MTATIRO AFICHUA KILICHOMFANYA AJIUNGE NA CUF

Naibu katibu mkuu wa CUF chama cha wanachi Mh.Julius Mtatiro,amebainisha kwamba  nchi inakuwa na viongozi mafisadi wengi kwa kuwa wengi hawana nia ya kuongoza ili kumkomboa mtanzanaia bali kukomboa matumbo yao.

Mh.Mtatiro aliamua kuweka wazi kile alichokiweka moyoni kwa muda mrefu kwamba kabla ya kujiunga na chama chochote cha siasa alifuatwa na vyama vyote vikubwa vya siasa hapa nchini wakimsahawishi ajiunge kwenye vyama vyao,lakini alivutiwa sana na ilani/itikadi ,sera ya CUF  kama alivyo tanabaishawa  na Prof.Lipumba (mwanyekiti wa CUF )  ambaye ambaye alifanya mazungumzo nae,  amabaye Mtatiro ansema yeye alikuwa tofauti na viongozi

Julius Mtatiro

Naibu Katibu mkuu wa CUF mh.Mtatiro akihutumia wananchi Ndungumbi,Makanya,Kinondoni

wa vyama vingine ambao walimuahidi,nyumba,gari,fedha na vyeo.”Hii haikuwa interest yangu mimi niliangalia chama gani chenye siasa za kweli na kinawatetea watanzania bila fix” alieleza Mtatiro.

Mtatiro pia ameonya tabia ya viongozi wa Chadema ya kununua viongozi wa CUF kwa fedha nyingi kama wanavyofanya CCM.Mtatiro alisema  kwamba tabia hii ianjenga viongozi wachumia tumbo na wasio na nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi ambao wengi wanakuwa mafisadi na wachumia matumbo.”Prof.Lipumba aliniambia -karibu CUF, hili ndilo neno ninalolikumbuka kwa kweli yeye ndiye aliyekuwa kiongozi pekee wa chama cha siasa ambaye hakujinadi kwa kutumia fedha.Kiufupi mimi huwezi kuninunua kama inavyofanyika kwa wengine kwani najitambua”aliongeza mh.Mtatiro

Naibu katibu mkuu huyo wa CUF aliendelea kutanabisha kwamba wanaushahidi wa sauti wa namna viongozi hao wa Chadema walivyokuwa wakihangaika kuwarubuni viongozi wa CUF mikoa ya kusuni kwa kutumia ahadi za kuwapatia  fedha pale watakapohama CUF na kuhamia Chadema wakati wa ziara yao ya mikoa ya kusini hivi karibuni.

Mh.Mtatiro alitanabaisha hayo juzi kwenye mkutano wa hadahara uliofanyika uliofanyika kata ya Ndugumbi Kinondoni ambapo kada muhimu wa CCM alihamia CUF na kushusaha bendera ya CCM kwenye tawi lake na kupandisha bendera ya CUF na kuunda tawi la CUF Mkombozi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s