CUF:HATUNA IMANI NA JESHI LA POLISI KUCHUNGUZA KUTEKWA DK.ULIMBOKA

Image

Dk.Ulimboka baada ya kuokotwa kwenye msitu wa Pande

CUF Chama cha wananchi   kimesema kimepokea kwa masikitiko makubwa juu unyama aliotendewa mwenyekiti wa  jumuiya ya madaktari nchini Dk.Steven Ulimboka .Taarifa hiyo imetolewa kwa vyombo vya habari na Naibu mkurugenzi wa uenezi,Habari na Haki za Binadamu.Mh.Abdul Kambaya.

Mh.Kambaya amesema kitendo cha kuuumizwa vibaya sana kwa DK.Steven Ulimboka ni kitendo ambacho hakikubaliki na nikinyume na kwa taifa ambalo tunadai tunalinda haki za binadamu.

Huu ni unyama mkubwa ambao unakila dalili za mkono wa serikli kwa ushahidi wa kimazingira kwamba msitu wa Pande uliotumiwa kumstesa Dk Ulimboka ulikwisha tumiwa na polisi kutesa na kuuwa wafanyabiashara wa madini mwaka 2006.

Pia kutokana na mgogoro wa madaktari na serikli na Dk.Ulimboka kuongoiza mgomo wa madaktari ambao serikali imepambana kuupinga bila shaka ni vigumu sana kwa serikli kukwepa uhusika wake kupitia jeshi la polisi.

Akielezea msimamao CUF-Chama cha Wananchi  ameaitaka serikali iunde tume ambayo haiusihi jeshi la polisi ili kuweza kupata matokea sahihi na yakuaminika juu ya tukio hili.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s