KERO ZA WATU WENYE ULEMAVU ZIZINGITIWE VILIVYO KWENYE SENSA NA KATIBA MPYA

CUF-Chama cha Wananchi kwa muda mrefu kimeendelea kufuatilia masuala mbalimbali ya haki za watu wenye ulemavu hapa nchini na kugundua kwamba kuna mambo mengi ambayo kwa muda mrefu pamoja  na  CUF kuendelea kuyapigania bado hayatiliwi mkazo wowote ikiwemo takwimu sahihi kulingana na makundi ya watu wenye ulemavu nchini, ambapo tunaona sasa  ni  vema zoezi la sensa linalotarajiwa kuanza mwezi Agosti mwaka huu likazingatia mahitaji ya kundi hili ikiwemo kufikiwa na kuhesabiwa.

CUF –Chama cha wanchi kinataka pia watu wenye ulemavu washirikishwe kikamilifu katika maandalizi ya  zoezi la sensa linalotegemea kuanza hivi karibuni, ili kuahakikisha kuwa wanayatambua kisahihi makundi yote yanayotambulika kwa sasa kama watu wenye ulemavu kwa hapa nchini, ili wakati wa zoezi la ukusanyaji wa takwimu iwe ni rahisi kaanisha katika madodoso yao.

Katika katiba mpya CUF Chama cha wananchi kinanatambua kwamba masula ya watu wenye ulemavu kuwa kwenye wizara ya Afya na ustawi wa jamii  ilikosewa na badala yake wanapaswa kuwa katika wizara inayohusu mambo mtambuka  kama vile ofisi ya waziri mkuu ama Ofisi ya rais kwani mambo ya walemavu mengi ni masuala mtambuka kama  vile elimu, afya, mawasiliano, miundombinu n.k.

Pia watu wenye ulemavu bado hawajawakilishwa ipasavyao kwenye ngazi mabalimbali za maamuzi jambo ambalo katiba  mpya inapaswa kulizingatia kwa makini ,na watanzana wote wanapaswa kutetea hili ili watu wenye ulemavu Tanzania wawe na uwakilishi sawa wengine kimaamuzi katika ngazi mbalimbali za maamuzi hapa nchini ili haki zao ziweze kulindwa ipasavyo, ikiwemo na kuingizwa katika mipango ya kimaendeleo kwa kuzingatia mahitaji muhimu kwa kundi hili.

CUF Chama cha wanachi kitahakikisha kinapambana ili kuhakikisha haki hizi zinaingizwa kwenye katiba mpya ili watu wenye ulemavu waweze kupata haki zao zinazostahili.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s