MTATIRO AMFUNGA KITANZI MSAJILI WA VYAMA JOHN TENDWA

cuf,mtatiro,msaada,gongo la mboto

Naibu katibu mkuu wa CUF Mh.Mtatiro akizungumza wanachama wa tawi la CUF

Kauli ya msajili wa vyama vya siasa kuwa atavifuta baadhi ya vyama vya mifukoni “pocket parties” ni ya kinafiki kwelikweli, ni kauli inayoudhi na kusikitisha na ofisi yake inapaswa kuchunguzwa kwa kuwa na dalili za ufisadi na rushwa katika usajili wa vyama hivyo. Tendwa alitoa kauli hiyo ofisini kwake jana, wakati wa hafla ya kukabidhi cheti cha usajili wa kudumu kwa Chama cha Kijamii (CCK).

Chanzo cha kuwepo vyama vya siasa vya mifukoni ni yeye mwenyewe msajili, kauli yake ya kutaka kuvifuta vyama hivyo inamsuta,haitekelezeki na inamtia aibu.

Taifa letu limefika mahali ambako watumishi ambao tumewakabidhi ofisi za umma wanaongea uongo hadharani ili kuudanganya umma na kuficha maovu ya ofisi za umma.

Kuna makusudi ya wazi yanayoambatana na ujanja na hadaa kubwa zinazofanywa na ofisi ya Tendwa huku yeye mwenyewe akihusika kwa asilimia mia moja katika kuhakikisha vyama dhaifu visivyo na vigezo vinasajiliwa.

Mkakati huu unafanywa kwa lengo la kuweka utitiri wa vyama ambao hugeuka kuwa mawakala wa kuisaidia CCM katika chaguzi.Ndiyo maana hata kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 kuna vyama kadhaa vilitangaza waziwazi kumuunga mkono Rais Kikwete na vikazunguka nchi kumpigia kampeni.

Leo “msajili wa vyama” anazunguka kuwahadaa watanzania kuwa atavifuta vyama hivyo, huu ni uzushi na uongo mkubwa. Tendwa hawezi kuvifuta vyama dhaifu alivyovisajili yeye mwenyewe ili kutekeleza mkakati wa kuisaidia CCM.

Tumechoka kuwa na uongozi wa kinafiki na wanaotumia ofisi za umma kwa ajili ya matumbo yao huku watanzania wakiteseka kwa umasikini wa kutisha.

CUF –Chama cha Wananchi tunataka Ofisi ya msajili wa vyama ichunguzwe, kuna mashaka makubwa na hata viashiria vya ufisadi katika usajili wa baadhi ya vyama vya mifukoni, TAKUKURU waingie kazini, Tendwa na ofisi yake wachunguzwe, bunge lifuatilie suala hili pia.
HAKI SAWA KWA WOTE
Imetolewa na

Julius Mtatiro,
Naibu katibu mkuu,
CUF-Chama cha wananchi Tanzania bara,

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s